MAJINA YA WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JKT 2018

JKT - Jeshi la Kujenga Taifa, limefanya uteuzi wa wanafunzi waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kutoka shule zote za Tanzania Bara kwa mwaka 2018, kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria.


mahitaji muhimu kwa wanaojiunga na jkt 2018

Share on WhatsApp

JKT

JKT limewapangia Makambi ya JKT watakayokwenda kupatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 01-10 June 2018.


Wahitimu hao, wamepangiwa katika Kambi za:-

JKT Rwamkoma – Mara

JKT Msange – Tabora

JKT Ruvu – Pwani

JKT Makutupora – Dodoma

JKT Mafinga – Iringa

JKT Mlale – Ruvuma

JKT Mgambo - TANGA 

JKT Maramba – Tanga

JKT Makuyuni – Arusha

JKT Bulombora

JKT Kanembwa

Nachingwea- Lindi 

JKT Mtabila – Kigoma



Aidha, wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities) wanatakiwa kuripoti kambi ya Ruvu JKT iliyopo mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia wa jamii hiyo.

 MAHITAJI MUHIMU KWA WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA 2018 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JKT

Vijana watakaochaguliwa watatakiwa kujigharamia nauli za kwenda na kurudi kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa wakiwa na vifaa vifuatavyo:


  1. Bukta ya rangi ya Dark blue yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini isiyo na zipu. Aidha bukta za wanawake zinatakiwa kuwa na lastic magotini.
  2. Raba za michezo zenye rangi ya kijani.
  3. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.
  4. Soksi ndefu za rangi nyeusi.
  5. Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangwa kwenye mikoa yenye baridi.
  6. Track Suit ya rangi ya kijana au bluu

Mkuu wa JKT anawakaribisha vijana wote walioteuliwa ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza Uzalendo, Umoja wa Kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha na Utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu.


Bofya Hapa kuona Orodha kamili ya majina ya vijana na makambi ya JKT waliyopangiwa>www.jkt.go.tz


Source:- JKT Tanzania
Share on WhatsApp